Jumamosi, 04 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wakenya Amkeni

(Imetafsiriwa)

Kenya, shamba la kikoloni, kwa mara nyingine imo katika mchafuko na mtikisiko kwa kuwa mchezo wa bahati nasibu wa kidemokrasia umezunguka nyuzi 360! Walioko madarakani na walioko barabarani wakiandamana wanalaumiana, huku madai yakielekezwa kwa Mswada wa  Kifedha wa 2024 ulioandaliwa kwa maelekezo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) (Business Daily, 28 Juni 2024)! Mswada huo unapendekeza mikakati ya kuzidisha ukusanyaji wa ushuru ambao unatajwa kuwa ni wenye kukandamiza na kuwadidimiza  raia katika umasikini zaidi! Licha ya Rais wa Kenya, Ruto kuandikia bunge ili kuuondosha , bado raia hawaja punguza hasira na kusitisha maandamano.

Ukweli ni kwamba Mswada huo ulikuwa tu ni sanduku la  Pandora. Umefichua kufeli kupindukia kwa nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali ya kisekula ya Kimagharibi sio tu nchini Kenya na Afrika kwa ujumla hata katika miji ya Kimagharibi kwa kuwa msingi wake ni kupatiliza na kupora rasilimali za wenyeji na kuwakandamiza watu kwa maagizo ya warasilimali wakubwa. Kila kitu na kila mtu ni mtumwa kwa maslahi ya mabwana wakoloni Wamagharibi. Hivyo basi, marais au watawala wote wapo kama wasimamizi wa shamba la kikoloni, mabaraza yao ni wasaidizi wao! Raia waliobakia ni wafanyakazi ndani ya mashamba! Haishangazi, hapa nchini Kenya tangu ‘uhuru bandia wa bendera’ mnamo 1963, bado tunazirudia sera na sheria zilizoandikwa na Wamagharibi ili kusimamia shamba! 

Suala na suluhisho msingi sio KUJIUZULU kwa serikali ya Kenya na kubadilisha nyingine. Chochote kinachofanana na hilo itakuwa ni mabadiliko ya kiviraka yaliyo na matokeo kama yanayo shuhudiwa hivi sasa. Njia mbadala ya kimsingi ni kubadilisha kikamilifu mfumo wa kirasilimali wa kisekula wa Kimagharibi na nidhamu zake ambazo utekelezaji wake unaleta majanga duniani kote hivi sasa. Unatakiwa kubadilishwa kwa mfumo unaochipuza kutoka kwa Muumba wa ulimwengu, mwanadamu na uhai ikimaanisha Allah (swt) sio Yesu, mtume wa Allah (swt).

Wacha nitoe mlinganisho; sote tunakubaliana kwamba pikipiki ili kuwaka tunahitaji petroli. Hata hivyo, tukisonga mbele na kutia ima maji au dizeli na kutarajia pikipiki kuwaka, itakwama kabisa na utadhaniwa kuwa mwendawazimu. Je, sisi sio wendawazimu kushiriki katika mchezo wa kidemokrasia ilhali Muumba wa ulimwengu, mwanadamu na uhai ana maamrisho ya wazi kuhusu namna gani tuweze kuendesha maisha yetu katika uhai huu mfupi?! Chaguo pekee la uhakika ni kukata mizizi ya mfumo wa kirasilimali wa kisekula na nidhamu zake na badala yake tujiunge na ulinganizi wa utekelezaji wa nidhamu ya Kiislamu kama inavyolinganiwa na chama cha kisiasa cha Kiislamu cha Kiulimwengu cha Hizb ut Tahrir. Mfumo wa Kiislamu na nidhamu zake zinapeana utulivu kwa watu wote pasina kuzingatia dini zao na viwango vya kiuchumi. Ni suluhisho pekee na mengine sio chochote bali ni natija ya akili yenye kikomo ya mwanadamu kwa mfano urasilimali, ukomunisti na ujamaa.

Lazima tuseme imetosha kushiriki mchezo wa bahati nasibu na unaoendeleza shida, mauaji, ukandamizaji na ukatishaji tamaa wanadamu na kupora rasilimali zao kupitia majambazi wachache! Tuamkeni na tuchukue hatua kwa kuachana na wakoloni Wamagharibi na mfumo wao na nidhamu zake!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro (Abu Taqiuddin)

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: « Hatuwezi Kuishi bila Mfumo wa Sasa wa Ulimwengu

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu