Jumamosi, 04 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

ICC: Ukumbi Kikaragosi wa Marekani wa Utoaji Haki

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 20 Mei, ICC ilitoa tamko ambapo Muendesha Mashtaka Karim A.A. Khan alisema kuwa “wameomba vibali vya kukamatwa katika hali kwenye nchi ya Palestina”. Vibali hivi vimetolewa kwa ajili ya kukamatwa Benjamin NETANYAHU na Yoav GALLANT kwa jinai kadhaa za kivita zilizotendwa dhidi ya watu wa Palestina. Hii ilikuwa ni sababu ya kusherehekea kote katika Ummah wa Kiislamu, walioamini kuwa hili ni jambo muhimu katika kuzuia mauaji ya ndugu zao Waislamu. Hata hivyo, imani hii sio sahihi kama ilivyothibitishwa na vitendo vya dola zenye nguvu za Kimagharibi, hasa Marekani.

Kufuatia kutolewa kwa tamko na ICC, viongozi kadhaa wa kisiasa wa Kimagharibi wametoa tamko la kushutumu hatua hizi, wakielezea vibali vilivyotolewa vya kukamatwa Mazayuni hawa wawili kuwa ni “mzaha”, “visivyokubalika”, na upotoshaji mkubwa wa haki”. Raisi wa Marekani Joe Biden ameelezea: “Acha niwe wazi: Chochote ambacho mwendesha mashtaka huyu anaweza kumaanisha, hakuna usawa – hakuna – kati ya Israel na Hamas”.

Pia, kiongozi wa Kizayuni ametamka, “Ninakataa katika hali ya uchukivu ulinganisho wa muendesha mashtaka wa The Hague baina ya Israel ya kidemokrasia na ya wauwaji wa umati wa Hamas”.

Hili limefuatiwa na kukataa kwa kiongozi wa Kizayuni kukubali masitisho kadhaa ya vita yaliyopendekezwa na UN na Marekani.

Kauli hizi zinathibitisha vitu viwili muhimu: 1. Umbile la Kizayuni halitosita wakati litakapokabiliana na mamlaka ya kimataifa. Na 2. Marekani itasimama bega kwa bega na umbile hili la kikoloni licha ya hukumu ya taasisi za kimataifa. Hii inatilia shaka juu ya nguvu ya mahakama namna hiyo.

Utafiti zaidi katika historia ya ICC unaonyesha kuwa kuna matukio kadhaa ambapo hukumu hazikukubaliwa na nchi kama Libya, Sudan, Ivory Coast na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo miongoni mwa nchi nyengine. Pia, utafiti juu ya kesi zilizoletwa mbele ya ICC unaonyesha kuwa hakuna mtu wa Ulaya wala Marekani aliyeweza kufunguliwa mashtaka. Hata kama upepelezi au uchunguzi wa awali ulifanyika, haya hayakupelekea kwenye mashtaka zaidi.

Kukosekana nguvu kwa ICC juu ya nchi kama Marekani kunaweza kuthibitishwa na vikwazo kadhaa ambavyo serikali ya Marekani imevipitisha dhidi ya ICC ambavyo vinajumuisha: kuzuia mali, vikwazo vya usafiri, na kuruhusu utumiaji nguvu dhidi ya The Hague kuwaachilia huru wafanyikazi wa Marekani kutoka kizuizi cha ICC.

Inafaa kutaja kuwa kukataa kwa Marekani kuruhusu ICC kuhukumu juu ya masuala yao pamoja na maafisa wa serikali wakieleza kuwa “Mfumo wa mahakama wa Marekani ni wenye uwezo wa kuendesha mambo yake yenyewe”. Hata hivyo, wakati Marekani inakataa kabisa kuruhusu ICC kuwahukumu wao au wale inaowaunga mkono, ina muda na wakati katika kuiunga mkono mahakama hiyo katika kesi dhidi ya nchi kama Libya, Sudan, na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kesi hizi zimemalizwa kwa vifo au kushikwa watu pamoja na mabadiliko yahusuyo usalama na utekelezaji.

Hatimaye, ili kuthibitisha nguvu iliyonayo Marekani juu ya ICC, na ICC kukosa nguvu, tunaweza kuangalia tukio la ICC la mwaka 2017 nchini Afghanistan. Muendesha mashtaka wa ICC aliomba kuchunguza tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu uliotendwa Afghanistan, ikiwemo matendo yaliotekelezwa na wanajeshi wa Marekani. Hili lilikabiliwa na upinzani mkubwa wa Marekani pamoja na vikwazo dhidi ya maafisa, akiwemo muendesha mashtaka aliyeomba kuchunguza uhalifu huo.

Ni wazi kuwa Marekani imehodhi nguvu zaidi ya zile za Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, zinazoiruhusu si tu kujiepusha na hukumu zake, lakini pia kulinda na kushambulia wale inaowaona wanafaa. Dola ya Kizayuni, licha ya mauaji ya halaiki ya waziwazi kwa watu wa Palestina, imeruhusiwa kuendelea na mauaji yake ya kikatili. Haya yote ni huku Marekani ikipiga kura ya turufu, kusambaza silaha za maangamizi, na kumpa kiongozi wao wa mauaji ya halaiki jukwaa la kujionyesha yeye na utawala wake kuwa ni waathirika.

Taasisi za kimataifa, ambazo zimesifiwa kwa kuleta haki, zimethibitisha kwa mara nyengine kuwa zinadhibitiwa na dola za kikoloni zikiwa na agenda za wazi. Ajenda hizi ikiwemo kuuangamiza Ummah na ardhi yake ili kunufaika na utajiri wake. Muda umewadia wa kuitisha suluhisho la usawa na haki kwa ndugu zetu Waislamu, na hii ni kwa kuunda dola ya Kiislamu. Dola isiyoruhusu dhulma na mauaji kuendelea bila kuadhibiwa ili kupata pesa zaidi. Dola isiyonunuliwa kwa vitu vya kimada, na itapinga ufisadi kote duniani.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Amatullah Hechmi

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu