Jumamosi, 04 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uzbekistan na Hizb ut Tahrir
(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo siku ya Ijumaa, Julai 5, 2024, Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir ilizindua kampeni ya kuwanusuru ndugu zetu wanaokandamizwa nchini Uzbekistan yenye kichwa: “Enyi Ummah... Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”

Maoni:

Mjadala kuhusu dawah ya Hizb ut Tahrir nchini Uzbekistan ni mpana; inagusia mwanzo, kuenea, dhulma, muhanga, na misimamo. Walakini, kwa uchache, ningependa kutoa maoni juu ya habari hii kwa vidokezi vifuatavyo:

Kwanza: Lau kama fikra za Hizb ut Tahrir zisingeenea sana nchini Uzbekistan, zisingekumbana na kiwango hiki cha kukamatwa na kuteswa, kwani maiti hapigwi vita.

Pili: Leo, ikiwa Uzbekistan itatajwa, mauaji ya Andijan yanakumbukwa, ambapo wafungwa na familia zao walipigwa risasi na kuzikwa chini ya lami. Ikiwa Uzbekistan itatajwa leo, magereza yanakumbukwa, ambapo wafungwa huchemshwa kwa maji hadi kufa shahidi, kama ilivyotokea kwa Usmanov, Mwenyezi Mungu amrehemu. Kung'oa meno, kuning'iniza wafungwa hewani kwa fimbo, kuwadunga wafungwa UKIMWI, kuwaziba pumzi kwa mifuko, na kuwatenganisha watoto wachanga na mama zao pia yatakumbukwa.

Ikitajwa Uzbekistan leo, maneno ya Bibi Inabethan Mwenyezi Mungu amrehemu, kwa wajukuu zake yanakumbukwa, kwani aliwausia wawe na subira katika kuubeba ulinganizi huu, akisema, “Hamtapata faraja kwa kutafuta faraja.” Kijana aliyeambiwa na mwandishi mmoja wa habari wa kigeni, “Unagawanya vipeperushi vya Hizb ut Tahrir kwa dolari 20,” alijibu kwa ujasiri, “Nitakupa dolari 100 na kukupa changamoto ya kugawanya vipeperushi vya Hizb ut Tahrir.” Pia anayekumbukwa ni yule kijana aliyefungua duka lake ili tu kupata mkate wake wa kila siku, na alipopata, alifunga duka na kwenda kutekeleza kazi ya ulinganizi (dawah).

Tatu: Mitihani na fitna ni Sunnah (sehemu ya maisha) iliyoasisiwa na Mwenyezi Mungu (swt) katika aya (aya) nyingi, kama vile kauli yake:

[لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ]

“Hapana shaka yoyote mtapata misukosuko katika mali zenu na nafsi zenu” [Surat Aal-i-Imran:186].

Hivyo ndivyo ilivyokuwa hali ya manabii na mitume, Maswahaba, na waliowafuata kwa wema.

«لَقَدْ كَانَ مَنْ قَبْلَكُمْ وَإِنَّ أَحَدَهُمْ لَتُحْفَرُ لَهُ الْحُفْرَةُ، ثُمَّ يُوضَعُ فِيهَا ثُمَّ يُوضَعُ الْمِنْشَارُ عَلَى رَأْسِهِ، ثُمَّ يُمْشَطُ بِأَمْشَاطِ الْحَدِيدِ مَا دُونَ عَظْمِهِ فَمَا يَصْرِفُهُ ذَلِكَ عَنْ دِينِهِ»

“Hakika waliokuwa kabla yenu alikuwa akikamatwa mtu na akachimbiwa shimo katika ardhi kisha ukaletwa msumeno juu ya kichwa chake akakatwa vipande viwili kisha akichanwa nyama za mwili wake kwa kichana cha chuma lakini hilo halikumuepusha na dini yake.”

Na ndivyo ilivyo leo kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa jumla na hasa viongozi wao.

Nne: Maumivu huisha, lakini ujira na malipo yanabaki kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Mtume (saw) amesema:

«...وَيُؤْتَى بِأَشَدِّ الْمُؤْمِنِينَ ضُرًّا وَبَلَاءً فَيُقَالُ: اغْمِسُوهُ غَمْسَةً فِي الْجَنَّةِ، فَيُغْمَسُ فِيهَا غَمْسَةً فَيُقَالُ لَهُ: أَيْ فُلَانُ، هَلْ أَصَابَكَ ضُرٌّ قَطُّ أَوْ بَلَاءٌ؟ فَيَقُولُ: مَا أَصَابَنِي قَطُّ ضُرٌّ وَلَا بَلَاءٌ»

“Basi ataletwa Muumini aliyepatwa na dhiki na taabu zaidi na itasemwa: ‘Mtumbukizeni Peponi, atatumbukizwa mara moja tu, kisha ataambiwa: ewe fulani je, umewahi kupatwa na madhara yoyote au taabu yoyote ile? Atasema: sipatwa na maradha wa taabu yoyote.”

Haya ni katika Akhera, lakini katika dunia hii, fikra za kukata tamaa wakati wa dhiki na matatizo zenyewe ni dalili za afueni iliyo karibu.

[حَتَّى إِذَا اسْتَيْأَسَ الرُّسُلُ وَظَنُّواْ أَنَّهُمْ قَدْ كُذِبُواْ جَاءهُمْ نَصْرُنَا]

“Hata Mitume walipo kata tamaa na wakaona kuwa wamekadhibishwa, hapo ikawajia nusura yetu,” [Yusuf:110].

Tano: Siku itakuja ambapo dhalimu jeuri atajuta yale aliyoyafanya, vilevile kesho Akhera

[وَلاَ تَحْسَبَنَّ اللهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الأَبْصَارُ * مُهْطِعِينَ مُقْنِعِي رُءُوسِهِمْ لاَ يَرْتَدُّ إِلَيْهِمْ طَرْفُهُمْ وَأَفْئِدَتُهُمْ هَوَاءٌ]

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao. Nao wako mbioni, vichwa juu, na macho hayapepesi, na nyoyo zao tupu.” [Ibrahim:42-43] au hapa ulimwenguni, kama ilivyotokea kwa afisa wa jeshi la magereza Hamza Al-Basyouni wakati wa enzi ya Gamal Abdel Nasser, ambaye alijulikana sana kwa kuwatesa wafungwa. Paji la uso wake lilitobolewa na vijiti vya chuma, vikapasua shingo yake na kugawanyika upande wake wa kulia hadi bega lake likatenganishwa na sehemu nyingine ya mwili wake.

Hatimaye, alfajiri ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume itadhihiri, hata kama makafiri, madhalimu na wajeuri wataichukia. Wakati huo, dhulma na giza vitaondolewa na nuru na uadilifu wa Uislamu. Kwa hiyo, tunawalingania, enyi Waislamu, kwa hili.

#صرخة_من_أوزبيكستان

#PleaFromUzbekistan

#ЎЗБЕКИСТОНДАН_ФАРЁД

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Jabir Abu Khatir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu