Jumamosi, 04 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Onyesho la Mshikamano nchini Malaysia huku Hali mjini Gaza Ikizidi kuwa Mbaya

(Imetafsiriwa)

Habari:

Hali mjini Gaza inazidi kuwa mbaya. Umbile haramu la Kiyahudi linaendelea na mashambulizi yake, na kusababisha idadi ya vifo ambayo sasa imefikia 37,000, na zaidi ya 82,000 kujeruhiwa. Inajulikana sana kuwa hakuna maeneo salama kabisa yaliyosalia kwa wakaazi wa Gaza kutafuta kimbilio kutokana na mashambulizi ya umbile hilo haramu la Kiyahudi. Takriban Waislamu wote wa Gaza sasa wanalazimika kuyahama makaazi yao, wakitafuta hifadhi hadi kusini mwa Rafah, karibu na mpaka wa Misri. Licha ya Umoja wa Mataifa kutoa azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano, umbile hilo la Kiyahudi linaendelea na mashambulizi yake yasiyokoma. Kwa kuzingatia hali mbaya inayowakabili Waislamu wa Gaza na Palestina kwa jumla, Hizb ut Tahrir Malaysia iliandaa maandamano ya amani mbele ya ubalozi wa Misri, Jordan na Marekani mnamo tarehe 14 na 21 Juni, tukisimama kwa mshikamano na ndugu na dada zetu nchini Palestina. Maandamano hayo yalipangwa ili kuishinikiza Misri na Jordan kutuma majeshi kukomesha mauaji ya halaiki na kuwaonya Wamarekani kuhusu adhabu ijayo kupitia kuibuka kwa Khilafah.

Maoni:

Hivi sasa, takriban wakaazi milioni 1.7 wa Gaza wamejazana katika khumusi moja tu ya eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza. Eneo hili, lililoteuliwa kwa madhumuni ya kibinadamu, bado halina mahitaji ya kimsingi, na maelfu ya watu wa Gaza wanaendelea kuuawa bila huruma na vikosi vya uvamizi. Wakati huo huo, Marekani inaendelea kuangazia nchi zinazozunguka umbile la Kiyahudi ili kuhakikisha kuwa wanajeshi wao hawaingilii mzozo wa Gaza. Marekani inafahamu hali tete, ambayo inaweza kubadilika bila kutarajia wakati wowote. Mauaji haya ya halaiki yameendelea kwa muda wa miezi minane, lakini umbile hilo haramu la Kiyahudi, likiwa na usaidizi kamili wa Marekani, bado halijafikia malengo yake na linakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wapiganaji wa Kiislamu wasio na vifaa vya kutosha huko Gaza. Hebu fikiria nini kingetokea ikiwa wanajeshi wa mataifa ya Kiislamu jirani na Palestina wangeingilia kati kuwatetea Watu wa Gaza! Hata hivyo, inaumiza moyo zaidi kwamba ikilinganishwa na hatua za sehemu kubwa ya jamii ya Magharibi, muitikio wa Waislamu kwa mauaji ya halaiki huko Gaza sio zaidi ya vuguvugu dhaifu. Kwa kweli, Waislamu wanapaswa kudhihirisha ulinzi mkubwa zaidi kwa Waislamu wa Gaza. Hii ni kwa sababu watu wa Gaza ni ndugu zao katika imani, na Gaza ni sehemu ya ardhi ya Waislamu. Hatua muhimu zaidi ambayo Waislamu ulimwenguni kote wanapaswa kuchukua ni kuwashinikiza watawala wao, haswa walio karibu na Palestina, kutuma haraka vikosi vya jeshi kuwahami na kuwalinda Waislamu wa Palestina, huku pia wakiendelea kufanya dua. Historia inadhihirisha jinsi makhalifa na wapiganaji waliopita walivyowalinda Waislamu kwa nguvu za kijeshi, wakisuluhisha kadhia kama hizo kwa mkato. Leo, Waislamu wanamhitaji sana 'Al-Mu'tasim' ambaye ataliamuru jeshi lake kuwahami Waislamu.

Sambamba na waraka uliowasilishwa kwa ubalozi wa Misri na Jordan, Waislamu kote ulimwenguni, haswa nchini Malaysia, lazima wachukue hatua zifuatazo kama juhudi kubwa pamoja na juhudi zengine zinazoendelea:

1. Wahimize wanajeshi wa Kiislamu na kuendelea kuwashinikiza viongozi wa Waislamu, hasa nchini Misri, Jordan, Saudi Arabia na Uturuki kuhamasisha majeshi yao. Viongozi hawa lazima wajikomboe kutoka kwa ushawishi wa Marekani na waache kuwa vibaraka wake, kuwasaliti Waislamu. Viongozi hawa wasaliti wanashuhudia moja kwa moja mauaji ya halaiki ya watu wa Gaza, wanasikia vilio vyao, na wanaona kufukuzwa kwao na mateso ya watoto na wanawake wao. Wahimizeni kupeleka majeshi ya Waislamu kuwaokoa Waislamu wa Gaza kutokana na mauaji ya halaiki, kuikomboa Palestina na kujikomboa nafsi zao kutokana na michezo ya kisiasa ya Marekani.

2. Toeni wito kwa viongozi kuchukua hatua madhubuti kwa kutuma majeshi na kuwashinikiza vikali wenzao kuhamasisha vikosi vya Waislamu kwenda Palestina. Inatosha kuwa watazamaji tu na wafuasi vipofu wa Marekani, na kusababisha kutochukua hatua katika kuokoa Waislamu wa Palestina. Umefika wakati kwa viongozi wa Waislamu duniani kote ikiwemo Malaysia kuacha kuipuuza Palestina ambayo imevuliwa utu na heshima yake tangu mwaka 1948.

3. Wahimizeni wanazuoni wa kidini kutoa fatwa za jihad ili kuitetea Palestina. Wito wa wanazuoni hao ni kuwakumbusha na kuwashinikiza viongozi kuchukua hatua za kivitendo na kuwafanya Waislamu wanyanyuke na kuchukua hatua madhubuti za kukomesha mateso na mauaji nchini Palestina.

4. Toeni wito kwa Waislamu wote kupitia vyama vya kisiasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, au watu binafsi kuchukua hatua za kivitendo zaidi pamoja na wanazuoni wanyoofu kuwatetea Waislamu wa Gaza. Haya ni pamoja na kufanya maandamano katika balozi za nchi zenye Waislamu wengi karibu na Palestina kuwashinikiza viongozi wao kukata mafungamano na Marekani na washirika wake. Wahimizeni Waislamu kunyanyuka na kutumia aina yoyote ya mashinikizo, ndani ya mipaka ya Sharia, mfululizo, hasa kwa viongozi wa Kiarabu na Uturuki hadi watakapokusanya majeshi yao kuwatetea Waislamu wa Palestina.

Waislamu lazima wachukue hatua ili kudhihirisha suluhisho la kweli la kutatua mzozo wa Gaza, ambalo ni Jihad fi Sabilillah. Ikiwa viongozi wa Waislamu wataendelea kuridhika, kuanguka kwao kutakuwa karibu na Khilafah inayokuja bila shaka itatangaza Jihad dhidi ya umbile la Kiyahudi lililolaaniwa!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad – Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu